Saturday, 24 December 2011

HOTUBA YA UCHAGUZI MKUU WA TASA

HOTUBA YA UCHAGUZI MKUU WA TASA-DELHI 28TH JAN 2012-UBALOZINI NEW DELHI INDIA. Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kumshukuru mwenyezi mungu kutukutanisha hapa sote,katika mkutano huu mkuu wa chama chetu cha tasa. Chama cha tasa-delhi ni chama cha wanafunzi wa kitanzania waliomo katika jimbo la delhi na viunga vyake,kisicho cha kiserikali wala kisiasa,kilianzishwa kwa lengo la kulinda maslahi ya wanachama wake,kuimarisha mahusiano ya wanafunzi wa kitanzania na kuimarisha umoja,utamaduni,na maendeleo ya kielimu na taifa kwa ujumla kwa wanafunzi. Malengo ya chama cha tasa ni kutoa ujuzi na uzoefu wa oungozi kwa wanafunzi wa kitanzania,vile vile kuoa ufahamu wa majukumu ya kijamii kwa wanafunzi,hivyo hutoa fursa kwa wanafunzi kushiriki ktk mambo ya kijamii na kujitolea. Madhumuni ya chama ni kuimarisha umoja,uelewa,mahusiano na kuendeleza ushirikiano wa kijamii na kitamaduni. Ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa wanafunzi wote ambao mmeweza kuitikia wito huu,mkaacha shughuli zenu zote,mkaja kujumuika pamoja katika kikao hiki nyeti kwa chama chetu. Kikao hiki ni muhimu kuliko vyote tulivyofanya ndani ya mwaka,kwani kinatuletea ukomo wa uongozi ulopita na kufungua ukurasa mpya wa uongozi ujao,pia kitatoa muhitasari wa yote yaliyofanyika,kushindwa na kufanikiwa kwa timu ya oungozi unaomalizia mda wake na hivyo kutoa mwongozo na changamoto kwa uongozi ujao. Ninapenda kuchukua fursa hii kutoa pongezi kwa balozi wetu hapa india...mh.eng.kijazi,kwa moyo wa upendo na wa kujitolea kwa hali na mali kwa wanafunzi na chama chetu kwa ujumla.balozi amekuwa mstari wa mbele kukisaidia chama hiki kimawazo na kiuchumi katika kuhakikisha kwamba chama hiki
kinafanikiwa kusonga mbele na kufikia malengo kusudiwa.nichukue fursa hii kwa niaba ya wanafunzi kuupongeza ubalozi na maafisa wa ubalozi ambao wamekuwa wakitutegea sikio pale tulipohitaji msaada wao,na kuwa tayari kuimarisha mahusiano ya pande hizo mbili. Niwashukuruni sana viongozi mbalimbali waliokuwa katika timu hii,kwa kujitolea kwa hali na mali katika kuendesha mipango mbalimbali ya chama.pia shukrani za pekee kwa viongozi tulioanza nao kazi lakini kwa sababu moja au nyingine walilazimika kutokuendelea na nafasi zao. Mnamo dec 2010,uongozi huu ulichaguliwa rasmi kuongoza shughuli mbali mbali za chama,katika kipindi kilicho kuwa kigumu katika historia ya chama chetu.kwanza kilikuwa kipindi ambacho kilikuwa na mipasuko na hali ya kutokuelewana kati ya wanachama.kipindi ambacho kilishuhudia matumizi ya anasa ya fedha za wanachama.tulianza safari yetu tukiwa na na wakati mgumu wa kuwaunganisha upya wanachama,kurejesha imani na kukirejesha chama katika barabara iliyokusudiwa kwa kufuata kipengere kimoja kimoja cha katiba yetu.
MAFANIKIO Tumefanikiwa kwa asilimia zote kuunganisha viongozi wote kufanya kazi kamatimu,,,kila kiongozi ana nafasi yake katika chama na siri ya mafanikio ni umoja na ushirikiano. Tumefanikiwa kuwaunganisha wanafunzi wa kitanzania wa delhi na viunga vyake vya karibu kama noida, na agra. Chama kimefanikiwa kukusanya kiasi kikubwa cha mapato kutoka kwa wanachama na kubudi vyanzo mbalimbali vya nje na vya ndani vya kimapato. Chama kimefanikiwa kuzuia mianya ya ubadhirifu wa fedha za chama...ambapo kila kiasi cha rs 5000 zitakazo kusanywa zitakabidhiwa ktk ofisi ya hazina ya ubalozi,,,,huku ipoti ya mhazini wa chama ikitolewa ktk kila robo/kikao.fedha hizo zitatolewa kwa idhini ya m/kiti+mhazin kwa pamoja. Chama kimefanikiwa kushiriki kwa njia moja ama nyingine ktk shughuli mbalmbali za kiutamaduni,kijami.chama chetu kimeweza kushiriki michezo ya nchi mbali mbai inayofanyika kila mwaka na pia wanafunzi wa kitanzania walipata mualiko rasmi kushiriki matamasha ya kiutamaduni ya kimataifa. Chama kimefanikiwa kuandaamatamasha mbalimbali ya kijamii kama gathering part,kutembelea wagojwa wa kitanzania mahospitalini kulingan na uwezo wa chama.na pia kushiriki shughuli za kitaifa, Chama kimefanikiwa kuunda rasmi nembo ya chama,na blog ya chama pia kufungua ukurasa wa chama ktk mtandao wa face book kwa nia na madhumuni ya kuimarisha umoja wetu,ushirikiana na kuwa karibu ktk kubadilishana mawazo. Chama kimefanikiwa kushiriki kikamilifu pindi matatizo,maradhi,na misiba inapotokea kwa wanachama...chama kama chama hutumia mfuko wake
kukopesha wanachama wanaotikiswa vibaya kifedha na kiuchumi mf,kuibiwa,kuugua au kufiwa...ktk mataizo yanayoletea mikusanyiko ya kijammii kwa mwanachama..chama kinakawaida ya ya kuchangia vitu kama vinywaji...uchangiaji huo hata hivyo hutegmeana na hali ya mfuko wa chama.
KUSHINDWA Pamoja na mafanikio mbalimbali ktk kukusanya mapato..zaidi ya 90% ya wanachama hawatoi ada ya chama..sio kwa sababu hawana,ila kwa sababu hawataki au hawajahamasika....kulingana na katiba mtu anyeshindwa kuchangia ada yake,mahudhurio chini75%--atabakia kuwa mwanachama asiye na sifa ya kupigia kura wala kufanya maamuzi ndani ya chama(non voting members)-unless ana matatizo ya kifedha. Japo kuwa tumekuwa tukipata mialiko mingi ya kiutamaduni,wanachama wengi hawana hamasa a kushiriki,,,wengi wanataka kuwa watizamaji,,,ni vyema tukawaiga wanachama wenzete wanaotokea ubalozini ambao` hujitolea ktk michezo yote hususani ya kiutamaduni,kwani sote ni jukumu letu. Tumependekeza kuandaliwa kwa jarida la chama litakaloelezea maisha,changomoto za wanafunzi india,jarida hilo litasambazwa maeneo mbalimbali nchini na ktk taasisi za kidiplomasia,,,wafadhili walikuwa tayari ila sisi tulishindwa kufanya maandalizi hayo... Tulishindwa kufanya picnic na utalii kutokana na mitihani ktk baadhi ya vyuo,uhaba wa fedha na maandalizi ya uhuru. Hitimisho Baada ya kusema hayo ni matumaini yangu kwamba uongozi ujao utaendeleza mbele pale tulipo malizia na hatimaye kutufikisha ktk chama cha watanzania halisi,chama kitakacholinda maslahi ya wanachama wake,bila kujali nafasi ya wasiopenda mafanikio yetu,bila kujali nafasi za walio na malengo ya kudharau viongozi wake na wanafuzi kwa ujula,chama kitakacho watupilia mbali wana utengano kwa na nia ya kuwaunganisha wanafunzi wa upande wa ubalozini na wale wa vyuoni na chama ambacho kitaongozwa uzalendo
badala ya manufaa binafsi,chama kitakacho wafanya watanzania wajisikie nyumbani na amani. Mwisho nitoe wito wa wanachama wote ,kwamba sisi sote ni ndugu,watnzaniak,tuendeleni kushirikiana na uongozi ujao,kwa hali,mawazo,ushauri na mali.ukionewa-usionee wasiliana na viongozi wa chama chetu,ukidhulumiwa waone viongozi kwanza kabla ya kujichukulia sheria mikononi, Shukrani za dhati tena viongozi wote wastaafu,ubalozi na wanachama wote kwa kutuunga mkono. Asanteni kwa usikilizaji wenu.

No comments:

Post a Comment